VICTOR TESHA AKISALIMIANA NA JOACHIM MTIMIA
Chama cha mapinduzi kimezidi kungara kwenye kampeni za serikali za mitaa huko kibosho mkoani kilimanjaro. Akizungumza toka huko chanzo cha habari hizi kinadai kuwa wananchi wamechoshwa na kelele za upinzani ambazo wamekuwa wakiwaomba kura ila wanapopewa huonyesha uwezo mdogo wa kuwahudumia wananchi. Katika kampeni za jana zilizoongozwa na kijana na kada wa CCM Victor Tesha zilimalizika kwa wakazi wa kibosho kuahidi ushindi mkubwa kwa wagombea wa CCM.
KIBOSHO
WAKAZI KIBOSHO WA KIBOSHO WAKIMLAKI VICTOR TESHA.
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya Mkutano Ndugu Victor Tesha alidai kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa ni kwa namna gani wanavyoweza kuwatumia viongozi walinaowachagua ili kujiletea maendeleo. Aliwataka pia wana CCM na viongozi wake waliopo Kibosho kuendelea na kampeni zenye utulivu kwani chama cha mapinduzi mojawapo ya misingi yake ni Amani.
Wananchi wakiagana na Ndugu Victor Tesha baada ya mkutano
Wananchi wakiagana na Ndugu Victor Tesha baada ya mkutano
Ndugu Victor Tesha akisalimiana na wakazi wa Kibosho baada ya Mkutano na kuwaaga.
Ndugu Victor Tesha akisalimiana na wakazi wa Kibosho baada ya Mkutano na kuwaaga.