Powered by Blogger.
Thursday, 29 January 2015
KIBOSHO MOSHI VIJIJINI CHADEMA YAPATA WAKATI MGUMU.
VICTOR TESHA AKISALIMIANA NA JOACHIM MTIMIA
Chama cha mapinduzi kimezidi kungara kwenye kampeni za serikali za mitaa huko kibosho mkoani kilimanjaro. Akizungumza toka huko chanzo cha habari hizi kinadai kuwa wananchi wamechoshwa na kelele za upinzani ambazo wamekuwa wakiwaomba kura ila wanapopewa huonyesha uwezo mdogo wa kuwahudumia wananchi. Katika kampeni za jana zilizoongozwa na kijana na kada wa CCM Victor Tesha zilimalizika kwa wakazi wa kibosho kuahidi ushindi mkubwa kwa wagombea wa CCM.
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya Mkutano Ndugu Victor Tesha alidai kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa ni kwa namna gani wanavyoweza kuwatumia viongozi walinaowachagua ili kujiletea maendeleo. Aliwataka pia wana CCM na viongozi wake waliopo Kibosho kuendelea na kampeni zenye utulivu kwani chama cha mapinduzi mojawapo ya misingi yake ni Amani.
Ndege iliyobeba silaha yakamatwa Nigeria
Halikopta mbili za kijeshi ni miongoni mwa zana za kivita zilizokamatwa kwenye ndege hizo ya mizigo.
Ndege ya mizigo iliyosheheni silaha za kivita imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kano nchini Nigeria.
Licha ya kukanusha awali, Urusi imesema inamiliki ndege ya mizigo iliyozuiwa katika uwanja wa ndege wa Kano kaskazini mwa Nigeria baada ya kugunduliwa imebeba silaha ambazo hazikuwa zimearifiwa.
Hata hivyo, Msemaji wa Ubalozi wa Urusi nchini Nigeria, ambaye aliliambia Shirika la Habari la Urusi TASS kwamba wanamiliki ndege hiyo, amesema silaha hizo ni za kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa BBC ndege hiyo bado inashikiliwa uwanjani hapo.
Awali, msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya kati aliiambia BBC kwamba hawafahamu chochote kuhusu helikopta mbili, magari ya kijeshi na silaha nyingine zilizokuwa katika ndege hiyo.
Hata hivyo baadaye alipiga simu kufuta usemo wake kwa kusema kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya wanajeshi wao, walioko katika kambi ya N’damena, ambazo zitapelekwa baadaye Ufaransa.
Msemaji wa Ubalozi wa Urusi mjini Abuja alisema pia ndege hiyo ni yao. Akitatanisha taarifa aliyoitoa awali kwamba ndege hiyo si yao.
Kwa nini Ufaransa inatumia ndege ya Urusi kubeba silaha zake? na kwa nini ilisimama katika uwanja wa Kano, wakati ikiwa inaelekea nchi jirani ya Chad na hata Cameroun ikitokea Afrika ya kati? Kwanini baadhi ya silaha hazikuorodheshwa katika ndege hiyo kama zimebebwa?.
Hayo ni maswali yalioulizwa pande zote.
Seriakli ya Nigeria ambayo ndio muhusika mkuu wa tukio hilo, haijasema chochote.
Baadhi ya wachambuzi wanasema Nigeria inamiliki silaha hizo ilizonunua katika soko haramu. Wengine wanasema silaha hizo zilinunuliwa kutoka kwa waasi wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya kati, wakielezea kwanini ndege hiyo imeingia nchini humo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Nigeria imewekewa vikwazo vya silaha kutoka Marekani na nchi hiyo imekuwa ikiarifiwa kutumia njia zisizo halali kupata silaha kwa ajili ya kupambana na wapiganaji wa Boko haram.
MTAFITI WA MASWALA YA NYOKA ANUSURIKA KUMEZWA NA “ANACONDA”
Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.
Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.
Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la Nyoka huyo.
Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya Anaconda mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka huyo.
Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa kichwa chake huku wenzake wakimtazama.
Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
“sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe sikutaka kujiumiza. ”
“nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi Nyoka huyo kwa vyovyote vile.”
”Mimi mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia jaribio vazi langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka huyo. ”
Lakini baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya tumbo la Nyoka na kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa angeumizwa na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa anaumizwa.
”Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe hapa.” alisema Paul.
Namna ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na Nyoka huyo bado ni muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake hilo kwa saa tatu.
Idris Sultan mshiriki wa mashindano ya Big Brother ‘hotshots’.Toka Tanzania ameibuka kidedea wa mashindano hayo yaliyokua yakifanyika nchi Afrika Kusini
Idris amekua Mtanzania wa pili kushinda shindano hilo ,baada ya Richard Dyle Bezuidenhout; kuibuka shujaa mwaka 2011 katika Big Brother II.
Mshindi huyu anajinyakulia donge nono la Dola za marekani laki tatu,kwa kuibuka mshindi.
Tayo Faniran toka Nigeria amekuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo .
Idris alitabiriwa na wapenzi wa kipindi cha Bigbrother kuwa angeweza kuibuka mshindi kutokana na wadau wengi kuvutiwa na namna alivyokuwa akiishi katika jumba hilo la big brother pia uhusiano wake na washiriki wenzake
TANZANIA SME Growth Center :YAAMUA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI.
Mkurugenzi wa Tanzania SME Growth Center VICTOR TESHA amesema ili makundi maalumu ya vijana na kina mama waweze kushiriki kattika kuinua uchumi wanapaswa kupewa mikopo ya riba nafuu. Akiyazungumza hayo wiliyani Moshi Vijijini mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja ndugu Tesha alisema kituo chake kimejipanga kuhakikisha vijana na kina mama wa Tanzania wanawezeshwa kimtaji.
Alisema SME imekuja na mikopo Mipya ambayo kina mama na Vijana waliopo kwenye Vikundi vya kuanzia watu 10 watakopeshwa mikopo ya vifaa kulingana na mradi wanaotaka kuunzisha. Amewataka vijana na kinamama kuchangamkia Fursa hiyo kwani ni mkpo wenye riba nafuu sana kuwahi kutolewa nchini ambapo wakopaji watarejesha kwa riba ya asilimia 5% ya mkopo walioukopa.
Mkurugenzi wa SME Victor Tesha Akiwaelekeza baadhi ya wananchi waliohudhuria semina maalumu ya ujasiriamali wilayani Moshi Vijijini.
Mkurugenzi wa SME Victor Tesha akiwaelekeza kinamama kwenye warsha namna ya kujikwamua kiuchumi wilayani Moshi Vijijini.
Mkurugenzi wa SME akipata maelekezo ya baadhi ya changamoto zinazowapata kina mama katika harakati za kujiletea maendeleo Wilayani moshi vijijini
Subscribe to:
Posts (Atom)